Waziri Mkuu Avamia tena Bandarini...Akuta Makontena 2431 Yametoka Bila Kulipiwa Kodi
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara nyingine ya kushtukiza bandarini na kukagua mfumo wa upokeaji na utoaji mizigo na utozaji wa m...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/12/waziri-mkuu-avamia-tena-bandariniakuta.html
WAZIRI MKUU Kassim
Majaliwa amefanya ziara nyingine ya kushtukiza bandarini na kukagua mfumo wa
upokeaji na utoaji mizigo na utozaji wa malipo baada ya kupewa taarifa kwamba
kuna makontena 2,431 yametolewa bila kulipiwa ushuru.
Waziri Mkuu alisema kwa mujibu wa taarifa ya ukaguzi wa bandari ya
kuanzia Machi hadi Septemba 2014, makontena hayo yalipita bila kulipiwa kodi
kupitia bandari kavu nne (ICDs) ambazo ni JEFAG, DICD, PMM na AZAM.
Kwa mujibu wa taarifa
hiyo, ni watumishi 10 tu ambao wamesimamishwa kazi kutokana na makosa
hayo.
“Mmeamua kuwasimamisha kazi watu wadogo na kuwaacha wakubwa wanaendelea na kazi. Hatuwezi kuendelea kuikosesha Serikali mapato namna hii,” alisema Waziri Mkuu.
“Mmeamua kuwasimamisha kazi watu wadogo na kuwaacha wakubwa wanaendelea na kazi. Hatuwezi kuendelea kuikosesha Serikali mapato namna hii,” alisema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu amemtaka
Kaimu Meneja wa Bandari, Bw. Hebel Mhanga amletee ofisini majina ya watumishi
wote waliohusika na ukwepaji kodi huo ifikapo leo saa 11 jioni.
Pia amempa Meneja huyo wiki moja kuhakikisha kuwa mamlaka hiyo inabadilisha mfumo wa utozaji malipo kutoka kwenye billing system na badala yake kuweka mfumo wa malipo wa kielektroniki (e-payment).
Pia amempa Meneja huyo wiki moja kuhakikisha kuwa mamlaka hiyo inabadilisha mfumo wa utozaji malipo kutoka kwenye billing system na badala yake kuweka mfumo wa malipo wa kielektroniki (e-payment).
Ametoa agizo hilo leo
(Alhamisi, Desemba 3, 2015), wakati akikagua idara mbalimbali za mamlaka ya
bandari na kuona ukaguzi wa mizigo unavyofanyika kwa kutumia scanners.
Akiwa kwenye chumba cha scanner mojawapo, Waziri Mkuu alikuta manifest moja ikisema kontena limejaa diapers lakini picha ya kwenye kompyuta ya scanner ilionyesha kuwa ndani ya kontena hilo kuna vitu kama vifaa vya umeme.

Kwa mujibu wa Kaimu
Meneja Bandari upande wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Ben Usaje ambaye
pia ni msimamizi wa kitengo cha scanner, inapobainika taarifa kama hiyo
inapaswa itumwe kwa wenye ICDs ili wafanye ukaguzi kwa kulifungua kontena ili
kuhakikisha mali zilizomo ndizo zilizoandikishwa kwenye manifest.
Katika hatua nyingine,
Waziri Mkuu Majaliwa amefanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi za Shirika la
Reli (TRL) na kukagua mabehewa yaliyokuwepo kisha akazungumza na baadhi ya
wafanyakazi waliokuwepo kwenye stesheni hiyo ambako alibaini madudu kwenye
malipo ya mishahara na makato ya michango ya wafanyakazi.
Akizungumza na
Mkurugenzi Mkuu TRL, Mhandisi Elias Mshana, Waziri Mkuu alisema amefika kwenye
shirika hilo ili kujifunza utendaji wao kazi lakini anazo taarifa za wao kupewa
fedha na Serikali kiasi cha sh. bilioni 13.5/- ili waendeleze miundombinu ya
reli lakini hawakufanya hivyo.
“Nia ya kuwapa fedha hizo ilikuwa ni kuboresha miradi ili muweze kujiendesha kibiashara lakini nyie mkaamua kujilipa wenyewe,” alisema.
“Nia ya kuwapa fedha hizo ilikuwa ni kuboresha miradi ili muweze kujiendesha kibiashara lakini nyie mkaamua kujilipa wenyewe,” alisema.
“Ninazo taarifa kuwa
baada ya hapo, mlikopa sh. bilioni 3 kutoka benki ya TIB ili kuendesha miradi
ya shirika lakini badala ya kufanya miradi, fedha hizo mkaamua nazo kujilipa
mishahara. Sasa sijui mnarudishaje huo mkopo wakati hakuna mradi wowote uliofanyika,” alihoji bila kupata majibu.
Alipoulizwa
wafanyakazi wana matatizo gani hapo TRL, Katibu wa TRAWU, Bw. Boaz Nyakeke
alisema wanadai malimbikizo ya makato yao kwenye mifuko ya pensheni,
malimbikizo ya makato kwenye SACCOS na malimbikizo ya kuanzia Julai – Novemba
2014.
Waziri Mkuu kwa upande
wake alimtaka Mhandisi Mshana asimamie uboreshaji huduma za usafiri wa treni
katika Jiji la Dar es Salaam ili hata mabasi ya mwendo kasi yatakapoanza
wananchi waweze kuwa na uhuru wa kuchagua aina ya usafiri wautakao.
“Tunataka kujenga yadi
kubwa nje ya mji ili watu wenye magari wawe wanayaacha huko na kutumia usafiri
wa treni au DART kuja mjini kama njia mojawapo ya kupunguza msongamano wa
magari jijini Dar es Salaam,” alisema.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
ALHAMISI, DESEMBA 3,
2015.