Baraza Jipya la Mawaziri Laiva
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam RAIS Dk. John Magufuli, wakati wowote anatarajiwa kutangaza Baraza la Mawaziri baada ya kukamilisha ...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/11/baraza-jipya-la-mawaziri-laiva.html
Na Mwandishi Wetu, Dar es
Salaam
RAIS Dk. John Magufuli,
wakati wowote anatarajiwa kutangaza Baraza la Mawaziri baada ya kukamilisha
wiki kadhaa za kuchuja majina ya wanaofaa kuwa mawaziri.
Hatua hiyo inakuja baada ya
juzi kukutana faragha kwa saa moja na Waziri Mkuu wake Kassim Majaliwa katika
kikao kilichofanyika ofisini kwa waziri huyo.
Katika kile kinachoonekana
ni tofauti na marais waliopita, ambao wengi wao walikuwa wakifuatwa ofisini,
hali imekuwa tofauti kwa Dk. Magufuli ambaye aliamua kwenda ofisini kwa Waziri
Mkuu Majaliwa na kufanya naye mazungumzo.
Chanzo chetu cha habari
kilipasha kuwa katika mazungumzo hayo kati ya Dk. Magufuli na Waziri Mkuu
Majaliwa pamoja na mambo mengine, walijadili hatua za mwisho za uteuzi wa
mawaziri ambao watakuwa tayari kufanya kazi kwa kujituma na wakati wote
kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.
“Sasa Baraza la Mawaziri
limeiva na kikao kati ya Rais Magufuli na Waziri Mkuu Majaliwa ni hatua ya
mwisho kabla ya uteuzi ambapo majina ya walioteuliwa yanaweza kutangazwa wakati
wowote kuanzia sasa.
“Mazungumzo yalikuwa marefu
kwa muda wa saa moja ambapo pamoja na kuweka mikakati ya Serikali ya awamu ya
tano, lakini pia suala la mawaziri lilichukua nafasi kwa wakuu hawa,” alisema
mtoa habari wetu.
Rais Magufuli, anatarajiwa
kuteua sura nyingi mpya huku baadhi ya mawaziri wa zamani huenda wakaangukia
pua kwa kutorudishwa tena kwenye baraza.
Hata hivyo, kiongozi huyo wa
Serikali ya awamu ya tano katika kampeni zake aliahidi kuteua baraza dogo la
mawaziri ambalo litakuwa na watu wachache wenye kujituma wakati wote.
Serikali ya awamu ya nne
chini ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ilimaliza muda wake Novemba 5, 2015 ikiwa
na Wizara 30 ambapo alipoingia kwa mara ya kwanza mwaka 2005, aliunda Baraza la
Mawaziri na naibu wao 60.
chanzo:Mtanzania
