Almasi Adimu Yagundulika Tanzania
KAMPUNI ya madini ya Petra Diamonds imegundua aina adimu ya almasi ya rangi ya pinki yenye uzito wa karati 23.16 kutoka mgodi wake wa Willi...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/12/almasi-adimu-yagundulika-tanzania.html
KAMPUNI ya madini ya Petra
Diamonds imegundua aina adimu ya almasi ya rangi ya pinki yenye uzito wa karati
23.16 kutoka mgodi wake wa Williamson uliopo Mwadui, Shinyanga.
Kwa
mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo ya madini, almasi hiyo ya pinki, moja ya
madini ya rangi yanayosakwa zaidi duniani ni mfano wa ubora wa hali ya juu na
ugunduzi mkubwa na muhimu zaidi kufanywa na Petra kutoka mgodi huo hadi sasa.
“Almasi
za pinki hupatikana katika migodi michache duniani na uadimu wake huzifanya
kuwa moja ya madini yenye rangi yanayotafutwa zaidi duniani,”taarifa ya kampuni
hiyo ilisema.
Rangi
ya pinki katika almasi inadhaniwa kuletwa kutokana na mabadiliko ya muundo wa
molekuli, ambao unaaminika kusababishwa na aina fulani ya mtikisiko wa ardhi
(seismic shock) unaotokea wakati wa kipindi cha uumbaji wa almasi.
Pande
hilo la almasi litauzwa katika mnada huko Antwerp nchini Ubelgiji Desemba mwaka
huu.
Jiwe
hilo jipya linasemekana kuwa na ubora zaidi kuliko almasi pinki yenye ubora wa
juu na uzito wa karati 16.4 iliyogunduliwa katika mgodi huo Septamba 2014,
ambayo iliuzwa kwa dola milioni 2.2 sawa na Tsh bilioni 4.7.
Novemba
10 mwaka huu, mteja mmoja wa China, ambaye hakuweza kutambulika alinunua almasi
ya pinki yenye umbo la mto na uzito wa karati 16.08 katika mnada huo kwa bei
iliyovunja rekodi ya dunia. Aliinunua kwa Pauni milioni 19 za Uingereza sawa na
Sh bilioni 61 za Tanzania kama zawadi kwa binti yake.
Katika
miaka karibu 250 ya historia ya minada, ni almasi tatu tu safi za pinki
zilizokuwa na uzito wa zaidi ya karati 10 zilizoonekana kwa mauzo, kwa mujibu
wa taasisi ya Christie’s.
