Walalamika Rais Magufuli kufuta Siku ya Ukimwi dakika za mwisho
Baadhi ya wadau wa Siku ya Ukimwi Duniani wamelalamika kupata hasara kubwa baada ya serikali kuyafuta, huku wakiwa tayari wameshafika m...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/11/walalamika-rais-magufuli-kufuta-siku-ya.html
Baadhi
ya wadau wa Siku ya Ukimwi Duniani wamelalamika kupata hasara kubwa baada ya
serikali kuyafuta, huku wakiwa tayari wameshafika mkoani Singida yalikokuwa
yafanyike kitaifa.
Wadau
hao ambao walikuwa washiriki maonyesho yaliyokuwa yaambatane na maadhimisho
hayo, wamedai hatua hiyo ya serikali pia itawasababisha wapate usumbufu na
matatizo makubwa wakati wa kurejea makwao, ikiwamo tatizo la nauli kwani baadhi
yao wametoka mikoa mbalimbali.
Wakizungumza
mjini hapa jana, wadau hao walisema wanapongeza hatua ya Rais Dk. John
Magufuli, kufuta maadhimisho hayo, lakini hatua hiyo ingefanyika mapema badala
ya kushitukiza hali iliyosawababishia usumbufu mkubwa.
“Hatua
ya Rais wetu ni nzuri kwa sababu dawa hospitalini zitapatikana kwa wingi,
lakini amaetushitukiza mno, angesema mapema ili tusije kabisa huku Singida,”
alisema Singu Hussein Singu, mjasiriamali wa tiba asilia kutoka mkoa wa
Kilimanjaro.
Akiunga
mkono kauli hiyo, Andrew Venance, mjasiriaamali wa tiba asilia kutoka Dar es
Salaam, alisema haelewi atarejeaje nyumbani kutokana na kuishiwa nauli baada ya
kutumia fedha nyingi kwa nauli na malazi.
Akizungumzia
malalamiko ya washiriki hao, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone, alisema
hatua hiyo ya Rais Dk. Magufuli itawasaidia wananchi wengi kupata dawa
hospitalini, hususani kwa waathirika wa virusi vya ukimwi.
Maadhimisho
ya Siku ya Ukimwi Duniani mwaka huu, ilikuwa yaanze Novemba 25 hadi Desemba
Mosi, mwaka huu mjini Singida.
Rais
Dk. Magufuli alipangwa kuwa mgeni rasmi wakati wa ufungaji wa maadhimisho
hayo.
