Sherehe 30 za Maadhimisho ya Kitaifa mikononi mwa Magufuli
Rais John Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa wakati alipomtembelea Ofisini kwa Majaliwa jijini Dar es salaa...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/11/sherehe-30-mikononi-mwa-magufuli.html
Rais John Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa wakati alipomtembelea Ofisini kwa Majaliwa jijini Dar es salaam jana na kufanya mazungumzo ya faragha kwa takribani saa moja kasha alizungumza na makatibu muhutasi wa waziri mkuu. Picha na OPM
Sherehe 30 za maadhimisho ya
kitaifa zinazofanyika nchini kila mwaka huenda ‘zikachinjwa’ kutokana na kasi
ya Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli ya kupunguza gharama na kubana
matumizi ya Serikali yasiyo ya lazima.
Kwa ufupi
Wasiwasi
wa kufutwa kwa maadhimisho hayo ya kitaifa umekuja baada ya Rais Magufuli juzi
kufuta maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani iliyopangwa kuadhimishwa Desemba
Mosi kabla ya hapo, alifuta sherehe za Uhuru ambazo zingefanyika Desemba 9.
Rais
aliagiza kuwa fedha zitakazotumika kwenye maadhimisho ya Siku ya Ukimwi
Duniani, zitumike kununua dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARV) na
zile za Siku ya Uhuru zitumike kwa usafi wa mazingira ili kupambana na kipindupindu.
Florence Majani, Mwananchi Dar es Salaam.
Sherehe 30 za maadhimisho ya kitaifa
zinazofanyika nchini kila mwaka huenda ‘zikachinjwa’ kutokana na kasi ya Rais
wa Awamu ya Tano,
Dk
John Magufuli ya kupunguza gharama na kubana matumizi ya Serikali yasiyo ya
lazima. Wasiwasi wa kufutwa kwa maadhimisho hayo ya kitaifa umekuja baada ya
Rais Magufuli juzi kufuta maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani iliyopangwa
kuadhimishwa Desemba Mosi kabla ya hapo, alifuta sherehe za Uhuru ambazo
zingefanyika Desemba 9.
Rais aliagiza kuwa fedha zitakazotumika kwenye
maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, zitumike kununua dawa za kufubaza makali
ya Virusi vya Ukimwi (ARV) na zile za Siku ya Uhuru zitumike kwa usafi wa
mazingira ili kupambana na kipindupindu.
Katika
mwendelezo huo, jana Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alipiga marufuku
utengenezaji na uchapishaji wa kadi za Krismasi na Mwaka Mpya kwa gharama za
Serikali.
Katika
taarifa yake, Balozi Sefue ameelekeza kuwa yeyote anayetaka kutengeneza au
kuchapisha kadi hizo, afanye hivyo kwa gharama zake na ameagiza fedha
zilizopangwa kugharamia utengenezaji na uchapishaji huo, zitumike kupunguza
madeni ambayo wizara, idara na taasisi za umma zinadaiwa na wananchi na
wazabuni waliotoa huduma kwao au zipelekwe katika matumizi mengine ya
kipaumbele.
Sherehe
sasa kwa vipaumbele Akizungumzia kufutwa kwa maadhimisho ya sherehe za kitaifa,
Sefue alisema Rais Magufuli amechukua hatua hiyo kwa mamlaka aliyonayo kisheria
na kuwa hatua hiyo si endelevu, bali kwa kuangalia vipaumbele.
Sheria
ya Sikukuu za Kitaifa (The Public Holidays Act, Cap 35), inampa Rais mamlaka ya
kutangaza siku yoyote kuwa sikukuu au mapumziko.
Kutokana
na sheria hiyo, ndiyo maana Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete alitangaza Novemba 5
mwaka huu, kuwa ya mapumziko katika kuhitimisha uongozi wa awamu ya nne na
kuukaribisha wa awamu ya tano.
“Maadhimisho
haya yana umuhimu lakini si lazima yafanyike kila mwaka, tunaweza kuamua mwaka
huu tufanye au turuke mwaka mmoja. Siku ya Ukimwi ina umuhimu na siku ya Uhuru
ina umuhimu pia, lakini tunapima kwa kuangalia wapi kuna mahitaji zaidi,”
alisema.
Alisema
uamuzi huo wa Rais ni njia mpya ya kupanga vipaumbele kutokana na hali halisi
ilivyo katika sekta zenye mahitaji makubwa na ya haraka.
Katika hotuba yake ya kuzindua Bunge ya
Novemba 20, Rais Magufuli alisema Serikali itadhibiti warsha, semina,
makongamano na matamasha ambayo yanatumia fedha nyingi za lakini hayana tija.
Alisema
atahakikisha kila senti inayoongezeka katika mapato ya Serikali inaelekezwa
katika kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi. “Tutaziba mianya ya upotevu wa
fedha za Serikali ambayo inaipunguzia Serikali uwezo wake wa kuwahudumia
wananchi,” alisema katika hotuba hiyo.
Baadhi
ya maeneo ambayo alisema yatasimamiwa ili kupunguza matumizi yasiyo ya lazima
na kuziba mianya ya uvujaji wa fedha za Serikali ni kufuta safari za nje, posho
za kujikimu na kodi.
Wazungumzia kasi ya Magufuli Hatua hiyo ya
Rais Magufuli, imepongezwa na baadhi ya wanasiasa na wanaharakati.
Aliyekuwa
mgombea wa ubunge wa Segerea, Julius Mtatiro alisema Rais alitakiwa kuandaa
utaratibu wa kufuta sherehe hizi kila mwaka ili fedha zitumike katika sekta
nyingine za kimaendeleo. “Niliposikia amefuta nilidhani ni kwa miaka yote kumbe
ni mwaka huu tu, inawezekana labda ni kwa sababu Serikali haina fedha na wala
si kupunguza matumizi yasiyo ya lazima,” alisema.
Alisema
sherehe hizo ni vyema zikafutwa kabisa kwani hazileti maana kutumia fedha
nyingi wakati wanawake wanajifungulia sakafuni na watoto wanaketi chini
madarasani.
Meneja Utafiti na Uchambuzi wa Sera wa
Hakielimu, Godfrey Bonaventure alipongeza hatua ya Rais Magufuli huku akitaka
hatua hiyo iwe endelevu.
“Afanye hivi miaka yote, tumekuwa na utaratibu
usiopendeza ambao Serikali inakuwa na matumizi yasiyo ya lazima,” alisema.
Alisema anachofanya Rais Magufuli ni kutumia kile kidogo kilichopo na
kukiwekeza katika maendeleo badala ya kutumika katika matumizi yasiyo na tija.
Bonaventure
alimtaka pia kufuta sherehe za kupongezana baada ya bajeti kupita na mambo
mengine yasiyo na msingi. “Masuala ya safari, semina, vikao na ‘overtime’ fedha
huwa zipo lakini masuala muhimu siku zote tunaambiwa fedha hazitoshi, kwa
nini?” alihoji Bonaventure.
chanzo:mwananchi
