Mohamed Dewji Ashinda Tuzo ya Mtu wa Mwaka(Person of the Year) ...METL Yaongoza Kutoa Ajira Sekta Binafsi
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mohamed Enterprises, Mohamed Dewji amesema kampuni yake inaongoza sekta binafsi kwa kutoa ajira k...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/11/mohamed-dewji-ashinda-tuzo-ya-mtu-wa.html
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mohamed Enterprises,
Mohamed Dewji amesema kampuni yake inaongoza sekta binafsi
kwa kutoa ajira kwa vijana. Kampuni hiyo pia inamiliki
mashamba makubwa ya mkonge yaliyopo katika mikoa ya Tanga, Morogoro
na Kilimanajaro. Dewji alisema kuwa ana kampuni 31 ambazo
zinatengeneza bidhaa mbalimbali za Kitanzania ambazo zinatoa
fursa ya ajira kwa vijana wengi. Alisema hayo baada ya
kutwaa tuzo ya ‘Person of The Year’ iliyotolewa na jarida maarufu duniani la
Forbes, huku akibainisha kuwa tuzo hiyo inaashiria namna utajiri wake umekuwa
kwa kasi kubwa katika kipindi kifupi.
Katika hotuba yake aliyoitoa baada ya kupokea tuzo hiyo,
alisema mafanikio yake yametokana na matumizi ya teknolojia ya juu inayomsaidia
kuendana na ushindani unaobadilika kila siku.
“Heshima hii haitokani na utajiri nilionao, bali ni ubora
wa bidhaa zinazotengenezwa na kampuni zangu kugusa maisha ya watu wa aina
zote,” alisema Dewji na kuongeza: “Nina viwanda 31 ambavyo vimekuwa
vikitengeneza bidhaa za Kitanzania na kuziuza kwa Watanzania kwa gharama nafuu
ya kuanzia dola 200
. Pia, Ulaya nina kiwanda cha kanga na vitenge ambacho
malighafi zake zote zinatoka Tanzania naingizia Serikali kipato kwa kulipa kodi
ipasavyo,” alisema.
Alisema alipata
maono ya utajiri wake hasa kutoka kwa baba yake, Ghulam Dewji na kumwita
mjasiriamali shujaa ambaye alianzia kwenye udereva wa malori hadi kufikia kuwa
milionea. Alisema baba yake alimshirikisha katika biashara tangu akiwa mdogo.
