Taarifa ya Upotevu wa Makontena Azam ICD Toka SSB Group of Companies

Kumekua na taarifa zinazosamabazwa katika mitandao ya kijamii kuwa Kapuni ya Bakhresa inahusika na upotevu wa Makontena 349 yaliyolipo...



Kumekua na taarifa zinazosamabazwa katika mitandao ya kijamii kuwa Kapuni ya Bakhresa inahusika na upotevu wa Makontena 349 yaliyolipotiwa hivi karibuni kuwa yametolewa bandarini bila kulipiwa ushuru.Taarifa hizo zilitolewa na Waziri Mkuu wakati wa ziara yake Bandari ya Dar es salaam hivi karibuni.

Uchunguzi wetu umeonyesha kuwa sio kweli kuwa kuna makontena yenye bidhaa zilizoingizwa na kampuni hiyo ama ni miongoni mwa makontena yaliyohusika na sakata hilo.Isipokua kumetokea upotevu wa makontena yaliyoingizwa nchini na  baadhi ya wafanyabiashara katika eneo la kuhifadhia makontena (ICD) linalomilikiwa na kampuni hiyo ya Azam ICD.

Aidha imebainika kuwa kuna uchunguzi unaofanywa na mamlaka ya mapato nchini TRA, huku kukiwa na ushirikiano na uongozi wa Kamapuni hiyo (SSB Group of Companies) kuhakikisha wale wote wanaohusika upotevu huo wanachukuliwa hatua na kodi yote ya serikali inalipwa na wamiliki wote wa makontena yaliyohusika katika upotevu huo wanawajibishwa.

SSB Group of Companies
Corporate Affairs Department

November 29 ,2015

Related

Kitaifa 4000372346066854963

Post a Comment

emo-but-icon

item