MSD yakarabati jengo la duka la dawa hospitali ya taifa Muhimbili

BOHARI ya Dawa (MSD) imejiimarisha na kuhahikisha inatekeleza kwa wakati agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuweka maduka ya dawa katik...


BOHARI ya Dawa (MSD) imejiimarisha na kuhahikisha inatekeleza kwa wakati agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuweka maduka ya dawa katika hospitali za rufaa na kanda nchini.

Katika kutekeleza agizo hilo MSD imeanza kwa kasi kubwa ya kukarabati jengo la duka la dawa katika  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), ambalo linatarajiwa kufunguliwa kesho.

Mwandishi wa habari hii alishuhudia jana kasi kubwa ya mafundi ujenzi wakikarabati  jengo hilo ambalo awali lilikuwa likitumika kama stoo ya kuhifadhi vitu mbalimbali vya hospitali hiyo.

Akizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni kuhusu ufunguzi wa maduka hayo, Mkurugenzi Mkuu wa  MSD, Laureane Bwanakunu alisema  agizo la Rais la kuitaka MSD kuanzisha duka la dawa karibu na hospitali limekuja wakati muafaka kwani  kwenye mpango mkakati wa miaka sita wa MSD tayari ilikuwa na mpango wa kufungua maduka hayo kwa ajili ya kusogeza huduma karibu a wananchi.

Alisema maduka ya MSD ambayo yatafunguliwa kwenye hospitali za rufaa na kanda yatafanya kazi masaa 24 na kuuza dawa na vifaa tiba  chini ya bei ya soko pia yatahudumia watu binafsi na wale waliopo kwenye taratibu za Bima ya afya kote nchini.

“Ili kudhibiti watumishi wasio waaminifu kuiba dawa MSD inafanya kazi za uagizaji, uhifadhi  na usambazaji kwa kutumia mfumo wa mtandao wa E9 na tangu mwaka wa fedha uliopita tumeanza kuziwekea alama ya GOT bidhaa zetu ikiwa ni pamoja na vidonge.” alisema Bwanakunu.  

Alisema vidonge ambavyo tayari vimewekewa nembo ya GOT vipo 45 na wanaendelea kuwapa maelekezo wazabuni ili vyote viwekwe alama hizo..,nembo ya serikali inaonekana kwenye dawa za serikali kama Diclofenac, moxillin, iprofloxacin, Contrimoxale,paracetamol,na magnesium.

Alisema wanatarajia kuanzisha huduma ya kutoa taarifa kwa njia ya simu pale wananchi watakapoona kuna wizi wa dawa za serikali na kwamba wananchi  wanaelimishwa kutoa taarifa pale wanapoona dawa za serikali mitaani.

Alisema, pamoja na serikali kuanza kupunguza deni lake linalodaiwa na MSD bado inadaiwa Sh.bilioni 53.



Related

Kitaifa 4556215454057390706

Post a Comment

emo-but-icon

item