Manispaa ya ILALA yaendesha zoezi la kuondoa ombaomba
Halmashauri ya Manispaa ya ILALA kupitia Idara ya Mendeleo ya Jamii na vijana imefanya zoezi maalum la kuondoa ombaomba katika manispaa...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/11/manispaa-ya-ilala-yaendesha-zoezi-la.html
Halmashauri ya Manispaa ya ILALA
kupitia Idara ya Mendeleo ya Jamii na vijana imefanya zoezi maalum la kuondoa
ombaomba katika manispaa hiyo kuanzia tarehe 30 ya mwezi uliopita.
Akizungumza na wadau mbalimbali
wa maendeleo na ustawi wa jamii wa Manispaa hiyo Mkurugenzi wa Manispaa hiyo
ISAYA MUNGURUMI amesema zoezi hilo litakuwa endelevu ili kuhakikisha kwamba
linakwisha kabisa na usafi wa jiji wa DSM unadumishwa.
MUNGURUMI amesema sheria
zimeshaanza kutumika kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani
ombaomba wanaozurura mitaani mchana na usiku na kuwatumikisha watoto kinyume
cha sheria.
Amebainisha
kwamba wazazi wanapaswa kushitakiwa kwa kuvunja sheria ya kutowapa watoto haki
zao za msingi pamoja na ulinzi na kuwafanyisha kazi kinyume cha taratibu katika
mazingira hatarishi na ya udhalilishwaji.
Aidha
Halmashauri hiyo imeunda kikosi kazi kwa ajili ya kumaliza tatizo hilo
kinachojumuisha wadau wa sekta mbalimbali zikiwemo
