Maelfu wahudhuria misa ya Papa Uganda
Papa Francis amesheherekea misa mbele ya umati mkubwa katika eneo moja takatifu nje ya mji mkuu wa Uganda Kampala. Mamia ya maelfu ...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/11/maelfu-wahudhuria-misa-ya-papa-uganda.html
Papa Francis amesheherekea misa mbele ya umati mkubwa
katika eneo moja takatifu nje ya mji mkuu wa Uganda Kampala.
Mamia ya maelfu ya watu walihudhuria ibada hiyo katika
eneo la tukio la mauaji ya wafuasi wengi wa dini ya kikristo mwishoni mwa karne
ya 19.
Wakati wa misa hiyo ,Papa Francis aliwaagiza Waganda
kutumia mfano wa mashahidi hao kuwakumbusha kuhusu maisha yao ya kila siku
kupitia kuwahudumia wazee,masikini na wale waliotorokwa.
Siku ya Jumapili Papa Francis atafanya ziara yake ya
mwisho nchini Jamhuri ya Afrika ya kati CAR.
