Watumishi wengine watatu wa TRA wasimamishwa kazi
Waziri Mkuu wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa hii leo amewasimamisha kazi watumishi wengine watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TR...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/11/watumishi-wengine-watatu-wa-tra.html
Waziri
Mkuu wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa hii leo amewasimamisha kazi watumishi
wengine watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao jana iliamriwa kwamba
watahamishiwa mikoani.
Mhe. Majaliwa amesema ili kupisha uchunguzi zaidi wa tuhuma
zinazowakabili watumishi Anangisye Mtafya, Nsajigwa Mwandengele na Bw. Robert
Nyoni kama ilivyo kwa wenzao sita waliosimamishwa kazi jana (akiwemo aliyekuwa
Kamishna Mkuu), nao pia hawaruhusiwi kusafiri kwenda nje ya nchi hadi uchunguzi
utakapokamilika.
Waziri mkuu amemuagiza Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Dkt. Philip
Mpango atekeleze maagizo hayo kwa kuwaandikia barua watumishi hao.
Jana mchana, waziri mkuu alifanya ziara ya kushtukiza kwenye
bandari ya Dar es Salaam akiwa na nia ya kukagua namna shughuli zinavyoendelea
kwenye bandari hiyo hasa kwenye maeneo ya kupokelea mizigo kutoka nje ya nchi
na kubaini upotevu wa makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 80/-.
