Rais Kikwete kuhutubia Bunge la Kenya
Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete atahutubia bunge la Kenya Jumanne wiki ijayo huku akiendelea kujiandaa kuondoka mamlakani. Kiong...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/10/rais-kikwete-kuhutubia-bunge-la-kenya.html
Kiongozi huyo atahutubia kikao cha pamoja cha Bunge la Kitaifa
na Bunge la Seneti katika majengo ya bunge jijini Nairobi.
Rais Kikwete atakuwa kiongozi wa pili wa taifa la nje kuhutubia
bunge Kenya. Aliyekuwa kiongozi wa Nigeria Goodluck Jonathan alikuwa kiongozi
wa kwanza kuhutubia bunge la Kenya Septemba 6, 2013.
Spika wa Bunge la Kitaifa Kenya Justin Muturi aliambia wabunge
Alhamisi kwamba Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amemwandikia akiomba ruhusa
kiongozi huyo mwenzake akubaliwe kuhutubu.
“Ningependa kuwajulisha kwamba, baada ya kufanya mashauriano,
Spika wa Seneti nami tumekubali ombi hilo,” Bw Muturi aliambia wabunge.
Kwa muda sasa, Rais Kikwete amekuwa akizunguka maeneo mbalimbali
ya Tanzania akiwaaga wananchi.
Uchaguzi mkuu nchini Tanzania utafanyika Oktoba 25.
Bw Kikwete aidha hatakuwa kiongozi wa kwanza kuhutubia bunge la
taifa jingine Afrika Mashariki.
Majuzi Agosti 10, 2015 Rais Kenyatta alihutubia bunge la Uganda
wakati wa ziara rasmi ya siku tatu.
