Walioshinda Nafasi za Ubunge watakiwa Kuwasilisha Vyeti Vyao
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limewataka wabunge wote wateule kuhakikisha wanapatiwa vyeti vya kuteuliwa kuwa wabunge vin...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/11/walioshinda-nafasi-za-ubunge-watakiwa.html
Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limewataka wabunge wote wateule
kuhakikisha wanapatiwa vyeti vya kuteuliwa kuwa
wabunge vinavyotolewa na wasimamizi wa uchaguzi ili waweze
kusajiliwa baada ya zoezi la kuapishwa kwa Rais mteule Dkt. JOHN MAGUFULI
tarehe 5 mwezi huu Jijini DSM.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini DSM Naibu Katibu wa bunge JOHN
JOEL amesema wabunge hao wanatakiwa kuwasili jijini DSM kuanzia Jumatano ijayo
ili waweze kushiriki zoezi la kuapishwa Rais mteule.
Hata hivyo JOEL
amesema tarehe ya kuanza kwa bunge haijafahamika lakini kutakuwa na shughuli
mbalimbali zitakazofanyika baada ya wabunge hao kusajiliwa.
