Tazama Video ya Mbowe Akijibu Malalamiko ya Viongozi wa NCCR-Mageuzi
MWENYEKITI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye pia ni mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananachi (UKAWA), ...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/09/tazama-video-ya-mbowe-akijibu.html
MWENYEKITI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambaye
pia ni mwenza wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananachi (UKAWA),
Freeman Mbowe amesema, wanaoleta chokochoko ndani ya umoja huo walitaka
upendeleao.
Kauli ya Mbowe inakuja siku mbili baada ya Makamu Mwenyekiti wa
NCCR-Mageuzi, Leticia Ghati Musore na katibu mkuu wa chama hicho Mosena
Nyambabe kudai kwamba “Chadema imejipa umiliki wa UKAWA.”
Wakizungumza mbele ya waandishi wa habari viongozi hao wa NCCR-Mageuzi
walimtuhumu mwenyekiti wao James Mbatia ‘kutekwa’ na Chadema na kwamba,
ameshindwa kukitetea chama chao kwa kile walichosema kumezwa katika umoja huo.
Akizungumza na waandishi jana, Mbowe alisema viongozi hao wana
jambo lingine nje ya yale waliyoyatamka hadharani na kwamba, kubwa ni kutaka
kupewa upendeleo wa kugombea majimbo licha ya kukosa sifa.
“Tulikubaliana kuwa ili chama kipewe jimbo tutaangalia matokeo
ya chama 2010, tutaangalia madiwani wa chama husika katika jimbo, mtandao wa
chama pia matokeo ya uchaguzi wa vijiji na mitaa 2014 pamoja na mtandao wa
ushindi wa mgombea” alisema Mbowe.
Mbowe alisema majimbo ambayo Nyambabe na Leticia wamekuwa
wakiyang’ang’aniwa kugombea licha ya kutokuwa na sifa ni Segerea la jijini Dar
es Salaam ambalo walipewa CUF na Jimbo la Serengeti lililopo Mara ambalo
limekabidhiwa kwa Chadema.
“Nyambabe alihitaji kugombea Jimbo la Serengeti ambako Chadema
ilishinda vijiji 38 lakini NCCR haikushinda hata kijiji kimoja katika uchaguzi
wa vijiji, Chadema ina madiwani 8 NCCR haina hata mmoja, Nyambabe amegombea
jimbo hilo mara mbili kwa vyama tofauti lakini hakupata hata asilimia 5,
tungempaje hapo?” alihoji Mbowe.
Kwa upande wa Musore, Mbowe alieleza kwamba mwanamama huyo
aliomba aachiwe kugombea katika Jimbo la Segerea ambako NCCR haina mtandao wa
ushindi wala nguvu “jambo hili UKAWA tulilipinga.”
“Musore tunamfahamu aliwahi kuwa diwani wetu Tarime, hakujijenga
wala kujenga NCCR, katika Jimbo la Segerea pia lakini akawa anataka tumzawadie
jimbo kama makamu mwenyekiti taifa, hapana! tunataka kushinda hatuwezi kufanya
uamuzi tunaojua wananchi wataukataa,”alisema Mbowe.
Hata hivyo alisema UKAWA bado wanaendelea na utatuzi wa migogoro
iliyojitokeza katika majimbo na kwamba mambo yatakuwa mazuri muda si mrefu.
“Huu ni muungano wa vyama vinne, lazima kutofautiana kuwepo
lakini kamwe hatuwezi kushindwa kuelewana katika maeneo machache yaliyobaki na
hivi tunavyoongea Profesa Baregu, Salum Mwalimu, Bashage na viongozi wa CUF
taifa wameelekea majimbo yenye shida,”alisema Mbowe.
Baadhi ya majimbo yaliyo na utata ni Mtwara Mjini, Kigamboni,
Itilima (Simiyu), Masasi, Mtama (Lindi), Ngara na Sikonge.
Msikilize Mbowe akiongea
Msikilize Mbowe akiongea
