Kesi ya Pembe za ndovu: Tanzania Yaipeleka Malawi Mahakamani
Tanzania imeisimamisha Malawi isiteketeze moto tani 2.6 ya pembe ya ndovu ilizonasa katika operesheni dhidi ya wawindaji haramu Shehena...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/09/kesi-ya-pembe-za-ndovu-tanzania.html
Shehena hiyo ya meno 800 ya ndovu ilinaswa na maafisa wa forodha
wa Malawi ilipokuwa ikiingizwa nchini Malawi.
Tanzania ilikimbia mahakamani ilikuizuia serikali ya Malawi
isiharibu ushahidi wake dhidi ya watuhumiwa waliokamatwa na kesi inaendelea.
Mkurugenzi
mkuu wa idara ya kuwalinda wanyama pori wa Malawi anasema kuwa inasikitisha mno
kuwa Tanzania imekwenda mahakamani kuizuia idara yake isiteketeza bidhaa hizo
haramu kwa miezi mitatu ijayo.
''Tulikuwa tayari kuchoma moto pembe hizo za ndovu ambayo
ingekuwa ishara kamili kuwa tunapanga mikakati kabambe ya kupambana na
walanguzi na wawindaji haramu ili kulinda ndovu wetu,''
''Sasa
hilo halitawezekana kwa sasa na hadi baada ya miezi mitatu ijayo'' alifoka
Bright Kumchedwa
Idadi ya ndovu imepungua kwa asilimia 50% tangu mwaka wa 1980
nchini Malawi kutokana na uwindaji haramu.
Nchini Tanzania Idadi ya ndovu imepungua kwa asilimia 60% katika
kipindi cha miaka mitano tu iliyopita.
Mwezi uliopita mahakama moja iliwapata na hatia kaka wawili raia
wa Malawi na hatia ya uwindaji haramu na ulanguzi wa pembe za ndovu.
Wawili
hao walipigwa faini ya dola elfu tano za Marekani $5,500 na mahakama ikaamuru
bidhaa hiyo ichomwe moto katika kipindi cha siku 20.
Lakini serikali ya Tanzania nayo ikakimbia mahakamani ilikuzuia
serikali ya Malawi isiteketeza pembe hizo ikidai kuwa itakosa ushahidi wowote
dhidi ya watuhumiwa wake wa uwindaji haramu.
Tatizo la uwindaji haramu umekithiri katika miaka ya hivi
karibuni kufuatia utashi mkubwa wa bidhaa hiyo inayoenzia katika mataifa ya
mashariki ya mbali na bara Asia.
Si
aghalabu kushuhudia familia nzima ya ndovu na faru wakiangamizwa katika mbuga
za wanyama pori barani Afrika ambako ndovu bado wapo.
Mwaka uliopita viongozi wa mataifa ya Botswana, Gabon, Chad na
Tanzania yaliafikiana kuthibiti uuzaji wa pembe za ndovu.




