NEC: Vyama vinavyokiuka maadili ya Uchaguzi Viripotiwe ndani ya Masaa 72
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imevitaka vyama vya siasa vinavy...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/09/nec-vyama-vinavyokiuka-maadili-ya.html
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC), imevitaka vyama vya siasa vinavyokiuka maadili ya uchaguzi viripotiwe
kwenye Kamati ya Maadili ya Uchaguzi Mkuu ndani ya saa 72 kuanzia muda wa
tukio.
Aidha, imesema licha ya kuwapo kwa adhabu za ukiukwaji wa maadili ya uchaguzi kamati iliyoundwa kusimamia maadili imepokea malalamiko mawili pekee.
Akifungua semina ya kamati ya maadili ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu ilioandaliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kushirikisha wajumbe kutoka vyama vinane vyenye wagombea wa urais, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za sheria za Tume, Emmanuel Kawishe, alisema bila kufanya hivyo kuna hatari ya kuongezeka kwa matukio ya uvunjaji wa maadili.
Alisema malalamiko mawili yaliyopelekwa kwenye kamati ya maadili ni ya chama kimoja kuingilia ratiba ya kampeni ya chama kingine pamoja na picha ya mgombea wa chama kimoja kubandikwa juu ya picha ya mgombea wa chama kingine.
Bila kuvitaja vyama vilivyopelekwa kwenye kamati hiyo, alisema vyama vyote vya siasa vilisaini makubaliano hayo hivyo vinatambua ukiukwaji huo lakini havipeleki malalamiko.
Alisema kamati hiyo inafanyakazi mpaka siku ya mwisho wa kampeni kwa kutoa maamuzi na adhabu.
Semina hiyo ilikuwa na lengo la kuwawezesha wajumbe wa kamati hiyo inayoundwa na mjumbe mmoja toka katika vyama vya siasa vyenye wagombea urais kutoa maamuzi bila kukiuka sheria kwa mujibu wa maadili waliyojiwekea.
Alisema UNDP imetafuta mtaalamu muelekezi kutoa ushauri kwa wajumbe hao wa kamati katika kutoa maamuzi kwa wagombea au vyama vitakavyowasilisha malalamiko.
Naye mjumbe wa kamati hiyo, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Dominata Rwechungura, alisema kamati itatoa maamuzi ikiwa wahusika watapeleka malalamiko na uamuzi kutolewa bila upendeleo.
Alisema ukiukwaji wa maadili upo kwa kiasi kikubwa, vitisho, chuki , jazba pamoja na taasisi za dini kuingilia mchakato wa uchaguzi.
Katika maadili hayo yaliyosainiwa na vyama vyote vyama vya siasa na wagombea, hairuhisiwi kufanya fujo au kusababisha vurugu ya aina yoyote katika mkutano wa chama kingine.
Aidha, hairuhusiwi kutumia lugha ya matusi, kashfa, kejeli, udhalilishaji na vitisho au lugha inayochochea uvunjaji wa amani au kuashiria ubaguzi wa kijinsia ,ulemavu au maumbile.
Kadhalika hairuhusiwi kubeba silaha yoyote, kubeba sanamu, kinyago au kitu chochote kinachodhalilisha, kukebehi au kufedhehesha chama kingine, kiongozi au serikali katika mikutano ya siasa pamoja na kuchafua au kubandua matangazo au picha za kampeni ya vyama vingine.
Maadili hayo pia yanakataza kufanya kampeni kwenye nyumba za ibada na kuhakikisha viongozi wa dini hawatumiwi kupiga kampeni