Tisa Wajeruhiwa Katika Vurugu za Uchaguzi Mbeya
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya, kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi, Ahmed Msangi Watu tisa wamejeruhiwa vibaya na magari mawil...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/09/tisa-wajeruhiwa-katika-vurugu-za.html
![]() |
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya, kamishna
msaidizi mwandamizi wa polisi, Ahmed Msangi
|
Watu tisa
wamejeruhiwa vibaya na magari mawili kuharibiwa katika vurugu ambazo zimetokea
jijini Mbeya zikihusisha wafuasi wa chama cha mapinduzi, CCM, na wafuasi wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA.
Tukio hilo limetokea baada ya msafara wa mgombea ubunge katika
jimbo la Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Mr. II Sugu kupita
jirani na mahali ulipokuwa ukifanyika mkutano wa mgombea ubunge wa CCM, Sambwe
Shitambala.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, kamishna
msaidizi mwandamizi wa polisi, Ahmed Msangi amesema vurugu hizo zimetokea
katika eneo la Mbata, kata ya Ghana jijini Mbeya wakati msafara wa mgombea
ubunge wa CHADEMA, Joseph Osmond Mbilinyi ukipita katika eneo hilo ukielekea
eneo la Nsowo kwa ajili ya kufanya kampeni.
Kuhusu hatua ambazo zinachukuliwa na jeshi la
polisi ili kuhakikisha kuwa kampeni za uchaguzi mkuu zinaendelea na kumalizika
kwa amani, kamanda Msangi anasema kuwa watuhumiwa wote bila kujali hadhi zao
watafikishwa mahakani wakati wowote baada ya majalada yao kupitiwa na
mwanasheria wa serikal
Aidha kamanda Msangi amevitaka vyama vyote
vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mkuu kuzingatia ratiba ya kampeni ambayo
imetolewa na tume ya taifa ya uchaguzi ili kuepusha migongano isiyokuwa ya
lazima ambayo pia inaweza kuhatarisha amani kwa jamii.
