Mabasi 138 yaendayo haraka yatua Dar
Mwezi mmoja baada ya kuanza kutolewa kwa mafunzo kwa madereva maalumu, awamu ya kwanza ya mabasi 138 ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/09/mabasi-138-yaendayo-haraka-yatua-dar.html
Mwezi mmoja baada ya kuanza kutolewa kwa mafunzo kwa madereva
maalumu, awamu ya kwanza ya mabasi 138 ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka
(Dart) imewasili nchini kutoka China.
Agosti 16, Serikali ilizindua mafunzo ya madereva 330 ambayo
yangetolewa kwa awamu tano ili kuwajengea uwezo wa kuyaendesha na kuwahudumia
wateja.
Akipokea mabasi hayo kwenye Bandari ya Dar es Salaam, Mkuu wa
Mkoa, Saidi Meck Sadiki alisema muda wowote kuanzia sasa wakazi jiji hilo ambao
mradi huo unatekelezwa wataanza kutumia usafiri wa mabasi yaendayo haraka.
“Tumefikia hatua nzuri. Naipongeza Kampuni ya Usafiri Dar es
Salaam, Rapid Transit (Uda-RT) kwa kuleta mabasi hayo ili yaanze kutoa huduma
ya usafiri katika kipindi cha mpito. Hii itasaidia kuondoa adha ya usafiri kwa
wakazi wa jiji hili,” alisema.
Alisema, kampuni hiyo imepewa jukumu la kutoa huduma hiyo kwa
kipindi cha mpito ili ipate uzoefu kabla zabuni kuusimamia mradi huo kwa
kipindi cha kudumu haijatangazwa. Alisema uzoefu itakaoupata utasaidia
kuiongezea ushindani na kampuni za nje.
Kampuni hiyo inaundwa kwa pamoja kati ya Shirika la Usafiri Dar
es Salaam (Uda) na wamiliki wa daladala baada ya mabasi yaliyokuwa yakitumia
njia zilizopitiwa na mradi huo kutakiwa kuondoka.
Sadiki alisema nauli itakayotumika itapangwa kwa ushirikiano wa
taasisi mbalimbali chini ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafirishaji wa Majini na
Nchi Kavu (Sumatra).
Akizungumzia mabasi hayo mapya, msemaji wa Uda-RT, Subri
Maburuki alibainisha kuwa mabasi yaliyoingia ni 101 ya mita 12 na ya mita 18 ni
37 na huduma ya usafiri kipindi cha mpito itaanza baada ya kukamilisha taratibu
za bandari.
“Tuliahidi kuwa mwezi wa tisa mabasi yatakuwa yamewasili na ni
kweli yamekuja. Pamoja na yale (mawili) ya kufundishia yatakuwa 140,”alisema Maburuki.
Alisema mabasi hayo ni mapya na yanakidhi viwango na ubora wa
miundombinu ya barabara ya mradi wa BRT kama walivyokubaliana
