TRA Yakusanya Bilioni 5 za Kodi ya Makontena 329....Wafanyakazi 35 Wasimamishwa Kazi
BAADA ya Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa kufanya ziara ya kushitukiza katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kubaini upotevu wa Makon...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/12/tra-yakusanya-bilioni-5-za-kodi-ya.html
BAADA ya Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa kufanya ziara ya
kushitukiza katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kubaini upotevu wa
Makontena 329, mapya yaibuka kwa Makampuni 43 kuhusika kukwepa kodi ya
Sh.Bilioni 12.6 katika Bandari Kavu inayomilikiwa na Said Salim Bakhressa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,
Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Philip Mpango
amesema kuwa kampuni hizo 43 zilipitishiwa Kontena katika Bandari Kavu ya Said
Salim Bakhressa na kutaka ndani ya siku sita kuanzia leo kampuni zote ziwe
zimeshalipia kodi kutokana na idadi ya kontena.
Dk. Mpango amesema katika kampuni ambazo zilizokwepa kodi ambazo
zilipitisha Kontena 329 wameshalipa zaidi ya Sh. Bilioni Tano(5) ambapo
wanatakiwa kulipa kodi iliyobaki kuweza kumaliza kodi ya Sh.Bilioni 12.6 kwa
kipindi alichoweka Rais Dk .John Pombe Magufuli.
Kampuni zilizokwepa Kodi ya mapato kwa makontena 329 ni Lotai
Steel Tanzania LTD yenye makontena 100,Tuff Tyres Centre Company kontena 58 Binslum
Tyres Company LTD, Kontena 33, Tifo Global Mart (Tanzania) Company Limited
Kontena 30,IPS Roofing Campany Ltd Kontena 20,Rashywheel Tyre Center Com.Ltd
Kontena 12, Kiungani Trading Company Ltd 10 Homing International Limited
Kontena 9, Red East Building Kontena Saba,Tybat Trading Co Ltd, Kontena
Tano,Zing Ent Ltd,Kotena Nne,Juma Kassem Abdul, Kontena Tatu, Salum Continental
Co.Kontena Mbili, Zuleha Abbas Ali Kotena Mbili na Snow Leopard Building
Kontena mbili na waliobaki walikuwa na kontena moja moja.
Hata hivyo TRA imewasimamisha kazi watu 35 wakiwemo 27
waliokamatwa katika geti namba tano ambao hadi sasa wanashikiliwa na polisi kwa
mahojiano na uchunguzi .
Aidha amewataka wafanyakazi kuwasilisha mali zao ili kuweza
kuangalia uwezo wake katika utumishi kama zinaendana na umiliki huo.
