Sugu Awataka Madiwani Wa Chadema Kufukuzana na ‘Kasi’ ya Magufuli
Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu amewataka madiwani wa jimbo hilo waliochaguliwa kwa tiketi ya Chadem...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/12/sugu-awataka-madiwani-wa-chadema.html
Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu amewataka madiwani wa jimbo hilo waliochaguliwa kwa tiketi ya Chadema kuhakikisha wanafanya kazi kubwa kushindana na kazi ya rais John Magufuli.
Sugu alitoa kauli hiyo hivi karibuni katika kikao cha kumchagua
diwani atakayewania nafasi ya Umeya kwa tiketi ya chama hicho.
Aliwataka madiwani hao kuchapa kazi na kuwafanya wananchi
kujivunia kasi ya maendeleo inayoletwa na Mbunge na Meya wa jiji hilo ili
wasitamani jimbo hilo lingeongozwa na wapinzani wao wa CCM.
“Hata CCM wenyewe wamebadilika, Magufuli anakwenda jalamba.
Hakutakuwa na vitu kama ambavyo mnaviwaza, tunaenda kufanya kazi za wananchi
ili wananchi wasitamani kwamba afadhali na hapa pangekuwa CCM. Waseme hata kama
Magufuli anaenda spidi na sisi Mbeya yetu Meya na Mbunge wanakwenda spidi.”
