Baraza la Mawaziri la Magufuli ni Balaa......Yadaiwa Kila Waziri Atatia Saini Kukubali Masharti Yaliyowekwa na Magufuli
Kusuasua kwa Rais John Magufuli, kutangaza Baraza la Mawaziri kunatokana na msimamo wake wa kuwachambua watu anaotarajia kuteua kati...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/12/baraza-la-mawaziri-la-magufuli-ni.html
Kusuasua kwa Rais John Magufuli, kutangaza Baraza la
Mawaziri kunatokana na msimamo wake wa kuwachambua watu anaotarajia kuteua
katika nafasi hiyo huku akiaandaa mikataba ya makubaliano itakayokuwa mwongozo
kwa mawaziri hao.
Nia ya Rais, hadi kufikia hatua hiyo imetafsiriwa kwamba anataka
kupata mawaziri ambao wataweza kwenda sambamba na kasi yake pamoja na
wawajibikaji.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),
kinaeleza kwamba kwa sasa Rais Magufuli, anasuasua kutangaza baraza lake
kutokana na kile kinachodaiwa ni kuandaa mikataba ambayo mawaziri baada ya
kuteuliwa watalazimika kuisoma kwa muda wa siku mbili kabla ya kukubali uteuzi
huo.
Chanzo hicho, kilieleza kwamba wale watakaokubali itabidi wasaini
mkataba huo ili kukukabiliana na matakwa ya mkataba huo.
“Kwa sasa huyu jamaa anaandaa mikataba kwa ajili ya kuwapatia
Mawaziri na Manaibu wake na wanatakiwa kuisoma ndani ya siku mbili na yeyote
atakayekubaliana na mkataba huyo atalazimika kuisaini.
“Mikataba ya Mawaziri na Manaibu inalenga kuwabana watumishi hao
na kukubaliana kuwa iwapo itatokea tatizo katika wizara husika wao watakuwa wa
kwanza kuwajibishwa.
“Mkataba unalenga kuwafanya Mawaziri hao na Manaibu wao
kuhakikisha wanafanya kazi kwa uaminifu, uadilifu, na kwa kujali maslahi ya
jamii,” kilisema chanzo hicho.
Pia kilisema mkataba huo unaonekana unamasharti kwamba endapo
siku mawaziri hao watajiingiza kwenye vitendo vya kifisadi au Wizara husika
kulaumiwa watalazimika kujiuzulu bila kubembelezwa huku mhusika akifishwa
kwenye vyombo vya sheria bila mjadala.
Aidha, chanzo hicho kiliongeza kuwa kwa sasa wabunge waliowengi
wanaogopa nafasi za uwaziri na unaibu kwa madai kuwa kasi ya Rais Magufuli ni
kubwa na inaweza kumtia hatiani mtumishi wakati wowote.
“Wabunge hao wanapata homa kubwa kutokana na hatua ya Rais Magufuli
na Waziri Mkuu Majaliwa kuonesha ushujaa wa ajabu kwa kuwashambulia vigogo
ambao wameshindikana katika vitendo vya ukwepa wa ulipaji kodi au kufanya
ubadhilifu katika maeneo mbalimbali ikiwemo bandari.
“Kitendo kinachofanywa na Rais Magufuli ni sawa na kumvua nguo
Kikwete (Rais Mstaafu Jakaya Kikwete) kwani kwa madudu ambayo yanaonekana
inaonesha wazi kuwa nchi haikuwa na kiongozi na kama ilikuwa na kiongozi basi
kiongozi huyo alikuwa na mkono wake.
“Sikiliza kijana haiwezekani nchi ikawa na wafanyabiashara
wakubwa na matajiri wakubwa wanaokwepa kodi huku kiongozi wa nchi kwa kujua ama
kutokujua anakaa nao meza moja kwa kuwapongeza kwa misaada kiduchu wanayotoa
katika jamii huku wafanya biashara hao wakiongeza wigo waliyonacho na
wasiyonacho jambo ambalo ni hatari,” kilisema.
Wakati huo huo kuna tetesi kuwa kutokana na kasi ya Rais
Magufuli kwa sasa ndani ya CCM kuna mvutano mkubwa ambapo wanataka kubadilisha
katiba ya chama hicho.
Mgongano uliopo kwa sasa ndani ya Chama ni kutaka kubadilisha
katiba ya chama hicho ili rais asiwe mwenyekiti wa chama.
“Hofu hiyo inatokana na kasi ya Rais Magufuli na inasemekana
akiwa mwenyekiti watendaji wote ambao wapo maofisini kihasara hasara watakuwa
na wakati mgumu zaidi.
“Mbali na hilo kwa sasa inaonesha wale watu ambao walikuwa
wanapatiwa madaraka kwa njia ya kulindana itakuwa hadithi kwani waliowengi
wanaweza kutimliwa,” kilisema chanzo
hicho.
