Serikali Yafuta Posho za Vikao.. Sasa Semina na Makongamano kufanyika online kwa Tele Conferencing
SERIKALI kupitia Menejimenti ya Utumishi wa Umma Ofisi ya Rais imesema haitagharamia gharama zozote za kuendesha vikao kazi na watendaj...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/11/serikali-yafuta-posho-za-vikao-sasa.html
SERIKALI kupitia Menejimenti ya Utumishi wa Umma Ofisi ya Rais
imesema haitagharamia gharama zozote za kuendesha vikao kazi na watendaji wake
kuanzia sasa, badala yake vikao hivyo vitaendeshwa kwa kutumia Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEHEMA).
Wahusika wakuu wa vikao kazi hivyo ni pamoja na Wakurugenzi,
Makatibu Tawala wa Mikoa na Maafisa Utumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam,
Florence Temba, Mkuu wa Kitengo cho Mawasiliano Serikalini na Katibu Mkuu Ofisi
ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, amesema kuwa, kupitia utaratibu huo
washiriki wa vikao hivyo watabaki katika maeneo ya kazi ambapo wataunganishwa
na mtandao wa pamoja kwa mfumo wa kuonana na kuongea uso kwa uso.
“Tulianzisha mfumo huo ili kupunguza gharama zisizo na ulazima
ambapo awali ilitakiwa kila kunapokuwa na kikao lazma watumishi wasafili kuja
Dar es Salaam kwaajili ya mkutano lakini kwa sasa tutatumia Video Conference
iliyounganishwa kwenye mikoa yote nchini. Tumeokoa gharama za nauli, mafuta,
chakula na malazi,” amesema Temba.
Temba ameeleza kuwa, hatua za utekelezaji wa teknolojia hiyo
ulianza kufanyika tangu mwishoni mwa mwaka 2013 hadi sasa ambapo umekamilika na
kufanyiwa majaribio yaliyofauli kwa kufanya mikutano kumi ambayo iliunganisha
mikoa yote kasoro mitatu ambayo ni mipya ambayo ni, Njombe, Geita na Simiyu.
Kuhusu miondombinu ya mawasiliano amewatoa hofu watumishi kwa
kusema: “Mfumo huo ni salama hakuna haja ya kuhofia kuhusu kukatika kwa
umeme au hali ya hewa kwani mpango huo unaratibiwa na serikali hivyo ikitokea
hali kama hiyo kutakuwepo na umeme wa ziada au kwa kutumia mkongo wa Taifa wa
mawasiliano.”
