Mkapa Amsifu Kikwete kwa UDOM
Raisi Mstaafu Mhe, Kikwete alipotemebelea Kituo cha Sayansi UDOM RAIS mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa amepongeza jitihada za...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/11/mkapa-amsifu-kikwete-kwa-udom.html
![]() |
| Raisi Mstaafu Mhe, Kikwete alipotemebelea Kituo cha Sayansi UDOM |
RAIS mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa amepongeza
jitihada za Rais wa Awamu ya Nne Jakaya Kikwete kwa kutekeleza kwa vitendo
dhana iliyokuwepo ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Mkapa, ambaye ni Mkuu wa Chuo hicho alisema dhana ya
ujenzi wa chuo hicho ilikuwepo tangu awamu ya uongozi wake lakini mara
alipoingia madarakani Rais mstaafu Kikwete akaitekeleza, jambo ambalo ni la
kupongezwa.
Aidha aliwaasa wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu hapa
nchini kutumia taaluma zao kujiajiri ili elimu yao itumike kuwanufaisha
Watanzania wote kwa maslahi ya taifa huku akijivunia mafanikio yaliyopatikana
katika chuo cha UDOM kwa kipindi cha miaka sita.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu hiho,
Balozi Augustine Mahiga aliwataka wanafunzi waliojiunga na chuo hicho na wale
wanaoendelea kutumia fursa zilizopo kujiimarisha kitaaluma na kuongeza ujuzi.
“Inawezekana vitabu havitoshi au maktaba haikidhi wingi
wa wanafunzi lakini huu ni ulimwengu wa e-books mkitumia vizuri teknolijia ya
google na nyinginezo ambazo walimu wenu wanazifahamu mtajikuta katika ulimwengu
tofauti katika upatikanaji wa mabadiliko mbalimbali iwe ni vitabu, majarida au
makala,” alisema.
Alisema chuo kinatambua changamoto zinazowakabili na
kimejenga mifumo mizuri na thabiti ya kuwezesha na kukuza mawasiliano na
majadiliano kati ya uongozi wa wanafunzi na menejimenti ya chuo. Alisema chuo
hicho ni mahali pa kuimarisha uzalendo na umoja wa taifa kutokana na wanafunzi
kuchanganyika kutoka sehemu mbalimbali za nchi.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Idris Kikula alisema
jumla ya wahitimu katika mahafali hayo ya sita ni 4,136, wakiwa ni katika ngazi
mbalimbali za cheti, stashahada, shahada ya kwanza, stashahada ya juu, shahada
za uzamili na shahada za uzamivu.
Alisema kati ya hao, stashahada na cheti ni 159 na
shahada ya kwanza ni 3,435 na shahada za juu ni 542. Profesa Kikula alisema
idadi ya wahitimu imeongezeka kulinganisha na mwaka 2014 ambapo jumla ya
wahitimu ilikuwa 3,949.
Alisema kwa upande wa shahada za juu hiyo ni idadi kubwa
tangu kuanzishwa kwa chuo ambapo mwaka 2014 idadi ilikuwa 383 kati ya hao
uzamivu walikuwa 14, idadi hiyo imekuwa ikiongezeka kila mwaka na kwamba tangu
kuanzishwa kwa chuo idadi ya wahitimu kuanzia mahafali ya kwanza 2010 ni
26,663.
“Pia tunajivunia kuongeza nguvu kazi kwani kati ya
wahitimu wa shahada ya uzamivu 20, wahitimu 15 ni walimu wa UDOM,” alisema
