Madiwani Wanne Chadema Wajitokeza Kugombea Umeya Kinondon

Madiwani wanne wa Chadema Manispaa ya Kinondoni wamejitokeza kuwania umeya. Madiwani hao ni Boniface Jacob (Ubungo), Pascal Manota (Ki...


Madiwani wanne wa Chadema Manispaa ya Kinondoni wamejitokeza
kuwania umeya. Madiwani hao ni Boniface Jacob (Ubungo), Pascal Manota (Kimara), Ndeshikurwa Tungaraza (Makongo) na Abunel Bariki (Mbweni), walichukua fomu jana Makao Makuu  ya Chadema yaliyopo Kinondoni.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu hiyo, Jacob alisema ana imani atapitishwa na chama chake kugombea nafasi na kikubwa atakachokifanya akipewa ridhaa ya kuwa meya ni kuhakikisha Kinondoni inakuwa manispaa ya mfano kwa usafi.

“Huu ni utashi niliyopewa na Mwenyezi Mungu kugombea nafasi hii. Nawahidi wakazi wa Kinondoni, endapo nikifanikiwa kuwa meya nitafanya kazi na kila mtu kwa staili ya utatu yaani utaalamu, uongozi na wananchi,” alisema Jacob.

Aliongeza kuwa endapo Manispaa ya Kinondoni itaongozwa na Chadema chini ya mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), watafanya mambo ambayo aliyekuwa mgombea wa urais Edward Lowassa angeyafanya endapo angekuwa rais.

Mgombea mwingine, Manota alisema endapo Chadema kitampitisha na kushinda nafasi hiyo, jambo la kwanza atakalolifanya ni kuhakikisha Manispaa ya Kinondoni inakusanya kodi kwa ufanisi ili iweze kujiendesha.

Kaimu Katibu wa Chadema Wilaya ya Kinondoni, Rose Moshi alisema mwisho wa kutoa na kupokea fomu kwa chama hicho ni leo na kwamba mchakato wa kupitisha jina moja la mgombea unatarajiwa kufanyika kesho.


Hata hivyo, Moshi hakuwa tayari kutaja gharama za fomu hizo zaidi aya kuwahimiza madiwani wengine kujitokeza katika kinyang’anyiro hicho ili kuleta ushindani na hatimaye Chadema kusimamisha meya bora.

chanzo:mwananchi

Related

Habari Mpya 4196533468471924525

Post a Comment

emo-but-icon

item