NEC: Matokeo Ya kura za Urais Yatabandikwa Vituoni Ili Kuondoa Malalamiko Ya Kura Kuibiwa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuanzia sasa itaanza kubandika matokeo ya kura za urais kwenye vituo vya kupigia kura katika Uc...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/09/nec-matokeo-ya-kura-za-urais.html
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuanzia sasa itaanza
kubandika matokeo ya kura za urais kwenye vituo vya kupigia kura katika
Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ili kuongeza uwazi na kupunguza malalamiko ya wizi
wa kura.
Mpango huo umeelezwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,
Jaji mstaafu Damian Lubuva alipozungumza na viongozi wa dini jijini Dar es
Salaam ambao walimueleza hoja hiyo kuwa moja ya vigezo vitakavyokamilisha
mchakato huo kwa amani na utulivu na kuwaridhisha wagombea na wafuasi wa vyama.
Alisema licha ya kubandikwa vituoni, utangazaji wa matokeo
utafanyika kama kawaida katika kila ngazi, udiwani kwenye kata, ubunge wilayani
na urais Tume makao makuu.
Jaji Lubuva aliwahi kunukuliwa siku za nyuma akisema kuwa “hakuna
haja ya kuwa na shaka wala kuandaa vijana wa kulinda vituo. Hakutakuwa na
nafasi hiyo kwa sababu kura zote zitahesabiwa na kubandikwa huko.
“Kila mtu atajua diwani gani kapata kura ngapi, na mbunge na
hata rais aliyemchagua. Itakuwa tofauti na zamani ambapo zilikuwa
zinasafirishwa na kuhesabiwa wilayani ambako watu wengine walidhani
yanabadilishwa,” alisema.
