Chadema, NCCR-Mageuzi washikana Mashati Vunjo
HALI ya Umoja wa Vyama vinne vya Upinzani (UKAWA), si shwari ndani ya Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, kutokana na Chama cha Demokras...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/09/chadema-nccr-mageuzi-washikana-mashati.html
HALI ya Umoja wa Vyama vinne vya Upinzani (UKAWA), si shwari
ndani ya Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, kutokana na Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) na NCCR-Mageuzi kushindwa kuheshimu makubaliano ya
kumsimamisha mgombea mmoja kwa kila kata.
Hali hiyo imekuja baada ya wagombea udiwani wa Chadema kukataa
kumuunga mkono mgombea ubunge wa jimbo hilo NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ambaye
amesimama chini ya mwavuli wa Ukawa kwa madai kuwa, amekiuka makubaliano ya
umoja huo.
Wagombea hao walikwenda mbali zaidi na kudai kuwa, katika
kipindi hiki cha kampeni, hawatamnadi mgombea ubunge wa Ukawa wakidai hata yeye
mgombea ubunge amekuwa akiwapiga vita wagombea udiwani wa Chadema.
Mmoja wa madiwani hao, ambaye ni mgombea wa kata ya Mamba
Kusini, Fredy Shayo, alisema hali hiyo imetokea baada ya vyama hivyo kushindwa
kuelewana katika makubaliano ya kusimamisha mgombea mmoja, ambapo Chadema na
NCCR-Mageuzi vimesimamisha wagombea wao wa udiwani kwenye kata zote 16 za jimbo
la Vunjo.
