TRL walipewa bil 13 ila miundo mbinu haikujengwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipofanya ziara ya kushtukiza leo Shirika la reli, amezungumza na Mkurugenzi Mkuu TRL, Mhandisi Elias Msha...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/12/trl-walipewa-bil-13-ila-miundo-mbinu.html
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipofanya ziara ya
kushtukiza leo Shirika la reli, amezungumza na Mkurugenzi Mkuu TRL, Mhandisi
Elias Mshana,
Waziri Mkuu alisema amefika kwenye shirika hilo ili kujifunza
utendaji wao kazi lakini anazo taarifa za wao
kupewa fedha na Serikali kiasi cha sh. bilioni 13.5/- ili
waendeleze miundombinu ya reli lakini hawakufanya hivyo.
“Nia ya kuwapa fedha hizo ilikuwa ni kuboresha miradi ili
muweze kujiendesha kibiashara lakini nyie mkaamua kujilipa wenyewe,” alisema.
“Ninazo taarifa kuwa baada ya hapo, mlikopa sh. bilioni 3
kutoka benki ya TIB ili kuendesha miradi ya shirika lakini badala ya kufanya
miradi, fedha hizo mkaamua nazo kujilipa mishahara. Sasa sijui mnarudishaje huo
mkopo wakati hakuna mradi wowote uliofanyika,” alihoji bila Waziri Mkuu kupata
majibu.
Alipoulizwa wafanyakazi wana matatizo gani hapo TRL,
Katibu wa TRAWU, Bw. Boaz Nyakeke alisema wanadai malimbikizo ya makato yao
kwenye mifuko ya pensheni, malimbikizo ya makato kwenye SACCOS na malimbikizo
ya kuanzia Julai – Novemba 2014.
Waziri Mkuu kwa upande wake alimtaka Mhandisi Mshana
asimamie uboreshaji huduma za usafiri wa treni katika Jiji la Dar es Salaam ili
hata mabasi ya mwendo kasi yatakapoanza wananchi waweze kuwa na uhuru wa
kuchagua aina ya usafiri wautakao.
“Tunataka kujenga yadi kubwa nje ya mji ili watu wenye
magari wawe wanayaacha huko na kutumia usafiri wa treni au DART kuja mjini kama
njia mojawapo ya kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es Salaam,” alisema.

