Gesi Inayozalishwa MADIMBA Mtwara Yatumika Chini ya Uzalishaji wake

Serikali imeshauriwa kuharakishakuongeza uzalishaji katika mitambo ya kuchakata na kusambaza gesi ya MADIMBA mkoani MTWARA ili wananchi...


Serikali imeshauriwa kuharakishakuongeza uzalishaji katika mitambo ya kuchakata na kusambaza gesi ya MADIMBA mkoani MTWARA ili wananchi waweze kuondokana na kero ya kukatika kwa umeme pamoja na kuibua fursa za uanzishwaji wa viwanda vingine

Hayo yameelezwa na wadau wa masuala ya gesi baada ya kutembelea katika mradi wa gesi asilia uliopo MADIMBA na 

kuelezwa kuwa kati ya gesi yote inayozalishwa eneo hilo ni chini ya robo ndio inayochukuliwa na TANESCO kwa ajili ya kuzalisha umeme wa KINYEREZI huku gesi nyingine ikibaki bila matumizi yeyote kwa sasa hali inayopelekea mtambo mmoja tuu kutumika kati ya mitambo mitatu iliyopo.

Mkufunzi wa masuala ya mafuta na gesi DEO MFUGALE amesema serikali inatakiwa kuhakikisha inaitumia mitambo yote mitatu iliyopo katika eneo la MADIMBA badala ya kutumia mtambo mmoja pekee.

Katika hatua nyingine uwepo wa mradi huu katika eneo la MADIMBA umewanufaisha wakazi wa vijiji vya jirani wanaonufaika na huduma ya maji safi na salama inayotolewa bure


Related

Kitaifa 3430650875311157341

Post a Comment

emo-but-icon

item