Gary Neville ateuliwa kuwa kocha mkuu wa Valencia
Beki wa zamani wa Manchester United na kocha wa kikosi cha kwanza cha timu ya taifa Wingereza, Gary Neville ameteuliwa kuwa kocha mku...
http://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/12/gary-neville-ateuliwa-kuwa-kocha-mkuu.html
Beki wa zamani wa Manchester
United na kocha wa kikosi cha kwanza cha timu ya taifa Wingereza, Gary Neville
ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Valencia inayoshiriki Ligi kuu ya
Hispania.
Gary Neville ameteuliwa
kocha mkuu kwa mkataba mfupi na ataongoza timu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu
huu.
Neville amechukua nafasi
hiyo baada ya siku chache zilizopita kutimuliwa kazi kwa aliyekuwa kocha mkuu
wa timu hiyo, Nuno Santo na sasa Gary Neville atafanya kazi na ndugu yake Phil
Neville ambaye atakuwa msaidizi wake.
Akizungumzia kuteuliwa
kwake, Neville amesema ni furaha kwake kupata nafasi katika timu hiyo na
atatumia uwezo wake kuifikisha mbali timu hiyo na amekuwa akiifatilia kwa muda
mrefu anafahamu nini wanahitaji.
“Nina furaha sana kuteuliwa
kuwa kocha hapa, nimeifahamu Valencia tangu nikiwa nacheza mpira najua
mashabiki wa timu hii wanahitaji vitu vizuri tutashirikiana pamoja kuweza
kuisaidia timu kufika mbali ina kikosi vizuri nataraji tutafanya vizuri,”
amesema Neville.
Nae Rais wa Valencia, Person
Layhoon Chan amesema wamemteua Neville kwa kutambua uwezo wake na wanaimani
ataifikisha timu yao mbali zaidi ya walipo sasa.
“Tuna furaha kumtambulisha
Neville kama kocha wetu mkuu ataeongoza timu hadi mwishoni kwa msimu,
tunatambua uwezo wake ni mzuri tunataraji mambo mazuri akishirikiana na wenzake
waliopo katika kikosi chetu,” amesema Chan.
Neville ataanza kibarua
chake siku ya Jumapili Desemba, 6 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi ya
Mabingwa Ulaya UEFA dhidi ya Lyon ya Ufaransa katika Uwanja wa Mestalla siku ya
Jumatano Desemba,9.
