Kingunge Ngombale Mwiru Avuliwa Ukamanda wa Baraza la Umoja wa Vijana CCM

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Baraza kuu la Umoja wa Vijana wa CCM lililokutana tarehe 15.08.2015 katika ukumb...

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Baraza kuu la Umoja wa Vijana wa CCM lililokutana tarehe 15.08.2015 katika ukumbi wa Julius Nyerere International convention centre, pamoja na mambo mengine liliazimia mambo yafutauo:-

1. Lilimvua Ukamanda Mkuu ndugu Kingunge Ngombale Mwiru. Maamuzi hayo yalitolewa kutokana na tabia na mwenendo wake wa hivi karibuni kuenda tofauti na maadili na taratibu za CCM.

Aidha kikao kimetoa mapendekezo kwa vikao vya Chama Cha Mapinduzi kuuangangalia upya uanachama wake na kuchukua hatua kubwa zaidi.

2. Kikao pia kiliunda timu ya kampeni ambayo itafanya kazi pamoja na kamati ya utekelezaji kuhakisha ushindi wa CCM kwa nafasi zote.

3. Kikao kimemshukuru Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwa hotuba nzuri ya ufunguzi wa Baraza na kikao kimeahidi kutekeleza maagizo na maelekezo ya hotuba hiyo kwa matendo.

Sixtus Raphael Mapunda
Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa


Related

Siasa 31975714476023491

Post a Comment

emo-but-icon

item