Waziri Mkuu Majaliwa Afanya Ziara ya Kushtukiza Bandarini.....Awafuta Kazi na Kuamuru Kukamatwa Kwa Maofisa Kibao wa TRA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amefanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam mapema leo...
https://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/11/waziri-mkuu-majaliwa-afanya-ziara-ya.html
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa
amefanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam mapema leo na
kubaini upotevu wa makontena 349.
Waziri Mkuu amebaini upotevu wa makontena hayo ambayo yana
thamani ya zaidi ya shilling bilioni 80, na kuagiza kufutwa kazi mara moja kwa
maafisa waliohusika na upotevu huo.
Majaliwa amewasimamisha kazi Kamishna wa Kodi, Tiagi Masamaki
pamona na Habibu Mpozya wa kitengo cha huduma kwa wateja.
Uamuzi huo wa Waziri Mkuu umekuja baada ya kubaini kuwa katika
kumbukumbu za Mamlaka ya Bandari kuna taarifa ya makontena 349 yenye thamani ya
shilingi bilioni 80 lakini taarifa hizo hazipo kwenye kumbukumbu ya Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA).
Waziri Mkuu ameelekeza Polisi kuwakamata maafisa wote
waliohusika na sakata hilo kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
