Kasi ya Magufuli Yazidi Kuwaweka Watendaji roho juu
Katika kile kinachoonekana ni kutaka kwenda na kasi ya rais wa awamu ya tano, Dk. John Magufuli, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Rada...
https://taarifayahabari360.blogspot.com/2015/11/kasi-ya-magufuli-yazidi-kuwaweka.html
Katika kile kinachoonekana
ni kutaka kwenda na kasi ya rais wa awamu ya tano, Dk. John Magufuli,
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Rada kata ya Majohe, Jimbo la Ukonga,
Abdallah Goma, amewatimua ofisini wajumbe watano wa mtaa na kuwataka waende
mitaani kukusanya kero zinazowakabili wananchi.
Mwenyekiti huyo aliamua
kuchukua hatua hiyo baada ya wananchi kulalamikia tabia ya wajumbe
hao kuwadai malipo wakati wanapokwenda kutaka huduma
katika ofisi hiyo, ikiwamo kuandikiwa barua ya utambulisho benki.
Goma aliyasema hayo
alipokuwa akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana kutokana na
mvutano uliojitokeza kati yake na wajumbe aliowatimua kugoma kutekeleza
agizo lake na kususia vikao.
Alisema baada ya
kuapishwa alipanga ratiba ya kila mjumbe kukaa ofisini kwa muda wa siku mbili,
lengo likiwa ni kubaini tabia zao, hivyo katika kipindi hicho malalamiko ya
lugha chafu, kudai malipo ya kuandika barua ya dhamana na utambulisho yalijitokeza.
Tumeamua kutoa huduma bure au kwa
kuchangia gharama kidogo ya uchapishaji lakini siyo lazima ikiwa
mwananchi hawezi kuchangia, alisema.
Alisema wajumbe
waliruhusiwa kukaa ofisini kabla ya serikali kuajiri Afisa Mtendaji wa
Mtaa, lakini kwasababu mtendaji ameshaajiriwa kazi ya wajumbe hao ni
kukusanya kero tu.
Mmoja wa wajumbe hao, Siwema
Makamba, alisema wao wanajitambua kuwa ni wajumbe halali waliochaguliwa
na wananchi na ni wajibu wao kuwatumikia kwa nguvu zao zote.
Alisema kitendo cha Mwenyekiti
kuwafukuza ofisini ni kuwadhalilisha ili yeye atumie fursa
hiyo kurudisha pesa zake alizotumia kwenye uchaguzi na kwamba siyo
haki kwa wao kwenda kuzunguka mitaani.
Changamoto ya ofisi ymtaa ni
kutokuwa na mawasiliano mazuri na kusababisha mvutano wetu na
mwenyekiti, tunapaswa kuondoa tafauti ili tufanye kazi za wananchi, alisema.
Mmoja wa wakazi wa mtaa wa
Rada, Maulid Janga alisema yeye amesikitishwa na kitendo cha
wajumbe kumlipisha Sh. 50,000 kwa ajili ya kuliinua baraza la mtaa kwenda
kushughulikia mgogoro wa mpaka.
Unajua hadi leo mgogoro
wa mpaka haujashughulikiwa na pesa zimeliwa hivi hivi
na wajanja, kama walijua hawawezi kutatua tatizo kwanini wachukue fedha
zangu, alisema kwa masikitiko.
Afisa Mtendaji wa kata ya
Majohe Serrda Chidaga, alisema yeye ameshangazwa na mvutano
wa wajumbe kungíangíania kukaa ofisini na kushindwa
kwenda mtaani kukusanya kero za wananchi.
Baraza la maendeleo la kata
(WDC) limekaa na kujadili suala hilo na kutoa maelekezo kuwa hawatakiwi kukaa
ofisini lakini nashangaa bado wanangíangíania, lazima hatua za kinidhamu
zichukuliwe ikibainika kuna maslahi binafsi,î alisema.
chanzo:ippmedia
